November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ewura yatakiwa kuhakikisha huduma bora za maji zinaendelea kupatikana Busega

Judith Ferdinand, Timesmajira Online,Busega

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),imetakiwa kuendelea kujisimamia Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Busega(BUSEWASA),ili kuhakikisha huduma bora za maji zinaendelea kupatikana kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Busega mkoani Simiyu Anna Gidarya, wakati wa mkutano wa kutafuta maoni kuhusu ombi la kurekebisha bei za maji na usafi wa mazingira kutoka BUSEWASA uliofanyika Mjini Lamadi, Wilayani Busega, leo Agosti 24,2023.

Mkuu wa Wilaya ya Busega Anna Gidarya akifungua mkutano wa EWURA wa kupokea maoni ya wadau ikiwamo wananchi wa Wilaya ya Busega, kuhusu ombi la marekebisho ya bei za Mamlaka ya Maji Busega uliofanyika mjini Lamadi leo Agosti 24,2023

Amesema Serikali inaamini EWURA katika utendaji mahiri wa mdhibiti hivyo ili kuhakikisha huduma za maji bora zinaendelea kupatikana na kwa wananchi wa Busega inapaswa kuendelea kuisimamia BUSEWASA kwa umakini.

Sanjari na hayo ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa Wilaya ya Busega kutoa maoni kwa uhuru kuhusu ombi la kurekebisha bei za maji na usafi wa mazingira kutoka Mamlaka ya Maji Busega

“Serikali imewaamini EWURA na kuwatuma hapa kupokea maoni yetu wana-Busega ili tuweze kupata bei za huduma ya maji na kuilinda Mamlaka yetu isife, hivyo niwasihi sana mtoe maoni kwa uwazi na bila woga,”amesisitiza.

Akimwamilisha Mkurugenzi Mkuu wa EWURA katika mkutano huo Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa George Mhina amesema kuwa EWURA itaendelea kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

Wakazi wa Busega na wadau mbalimbali wakishiriki mkutano wa taftishi kuhusu ombi la marekebisho ya bei za maji kutoka Mamlaka ya Maji Busega ( BUSEWASA) uliofanyika mjini Lamadi leo Agosti 24,2023

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Busega Mhandisi Romanus Thomas, ameeleza sababu za kuomba marekebisho ya bei za maji ni kuongeza mtandao wa usambazaji huduma za majisafi na usafi wa mazingira, kuongezeka kwa gharama za uendeshaji ikiwamo gharama za umeme na kutibu maji.