Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Iringa
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Modeatus Lumato,amesema kuwa wamejipanga kupokea na kutatua malalamiko ya watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji ili wananchi wapate thamani halisi ya huduma zinazodhibitiwa
Hayo ameyasema leo Novemba 10,2022 wakati akishiriki kutoa elimu ya udhibiti wa huduma katika maonesho ya “Utalii Karibu Kusini 2022” yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa Kilolo, Mkoani Iringa.
Mhandisi. Lumato amewahakikishia wananchi wa Iringa na mikoa ya jirani kuwa EWURA ipo kwa ajili yao hivyo kuwataka wawe huru kuwasilisha malalamiko yao kutokana na huduma za umeme, mafuta, gesi na maji.
“Lengo letu ni kuhakikisha huduma zinazodhibitiwa zinapatikana kwa ubora na bei stahiki” ameeleza Mhandisi Lumato
Aidha, Mhandisi. Lumato ametoa wito kwa EWURA CCC kuendelea kuelimisha wananchi ili wajue haki na wajibu wao wakati wa kupata huduma zinazodhibitiwa.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inashiriki katika Maonesho ya kuhamasisha utalii wa maeneo ya Nyanda za Juu Kusini yaliyoanza Novemba 9 mpaka Novemba 12,2022 mwaka huu.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakani
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best