Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya(EU) imewataka jamii kuendelea utamaduni wa vyakula vya asili, ili kuboresha lishe bora na kuepuka na tatizo la udumavu kwa watoto.
Pia wamewataka wazazi kuwafundisha watoto kupika vyakula vya asili ili kuondokana na utamaduni wa kupenda vyakula vya kisasa.
Akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha la ‘Msosi Asilia’ linalolenga kuhamasisha ulaji vyakula vya asili iliyofanyika jana Temeke Jijini Dar es Salaam Mwakilishi wa Balozi wa EU,Anna Constine,alisema EU itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania kuhakikisha jamii zinatumia vyakula vya asili kwaajili ya kujenga afya.
“Tunashirikiana na Tanzania na FAO ili kuendelea kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili kwasabu vinaleta nguvu zaidi ukilinganisha na vyakula vingine vya kisasa,”alisema
Naye Afisa Kilimo Mkúu kutoka Wizara ya Kilimo,Magreth Natai alisema,serikali inaendelea kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula(FAO) kuhakikisha Watanzania wanaachana na ulaji wa vyakula visivyofaa na kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
“Wizara ya Kilimo tunaendelea kuhamsisha ulaji wa vyakula vya asili kila Mkoa kwasababu vinavirutubishi vyakutosha,tatakuwa na mbinu mbalimbali.’
Alisema serikali itaendelea kushirikiana na mradi wa Agriconnect kupitia EU kuendelea kuhamasisha jamii, ili kukabiliana na tatizo la udumavu na utapiamlo nchini.
Naye Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa FAO Charles Tulahi,alisema kampeni ya ulaji vyakula vya asili inalenga kukabiliana na tatizo la lishe nchini.Pia Tolahi ametoa rai kwa watafiti kuendelea kutafiti na kuzalisha mbegu za asili.Alisema FAO imeongeza kasi kuhamasisha ulaji vyakula vya asili kukabiliana na tatizo la utapiamlo katika nchi za Afrika.
AGRITHAMANINaye Mkurugenzi wa Taasisi ya Agrithamani Foundation ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Mashirika yasiyo ya Kiserikali(NGos) Neema Lugangira, alisema vyakula vya asili ndio vina viini lishe vya kutosha na vinamsaidia mtu kupata kinga.Neema alisema tamasha hilo litakuwa endelevu Kila mwaka na litakuwa linafanyoka katika mkoa wa Mbeya na visiwani Zanzibar.
“Huu ni sehemu ya mradi wa Agriconnect ambao uko chini ya Wizara ya Kilimo FAO na EU,na lengo ni kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili ndio tumeanza na tutafanya Mbeya na Zanzibar,”alisema
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best