Na Penina Malundo,Timesmajira
KAMPUNI ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Kusafirisha na Kusambaza Umeme(ETDCO)imekamilisha rasmi mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 132 kutoka Kata ya Ipole Wilayani Sikonge Mkoani Tabora hadi Kata Inyonga wilayani Mlele Mkoani Katavi.
Akizungumza mwishoni mwa wiki baada ya kukamilisha kwa mradi huo,Kaimu Meneja Mkuu wa ETDCO,CPA.Sadock Mugendi amesema baada ya kukamilika kwa mradi huo ndani ya siku mbili wananchi wataanza kupata umeme wa Gridi ya taifa.
Amesema kazi yao ni kuhakikisha umeme umetoka Tabora mjini mpaka katika Kituo Kidogo cha kupokea umeme (Substation) ya Inyonga ambapo zoezi tayari limekamilika na line sasa zinapitisha umeme.
“‘Rai yetu kwa wananchi kuendelea kutunza miundombinu ya umeme kwasababu,Serikali inatumia nguvu na fedha nyingi kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo,” amesema
Mhandisi CPA.Mugendi Mhandisi Dismass Massawe Kaimu Mkurugenzi huduma za Ufundi wa ETDCO amesema line hiyo itakapowasha itakaa kwa kipindi kisichopungua masaa 48 baadae watawasha Transfoma za substation nazo zitakaa katika kipindi cha majaribio ambapo baadae sasa watawasha umeme katika line zinazopeleka umeme kwa wateja.
Amesema wananchi wa Inyoga pamoja na majimoto watapata umeme kutoka katika kituo chao cha Inyonga hivi karibuni.
”Tunaelewa wote maeneo ya majimoto ni maeneo ambayo yanamashamba mengi na mpunga na shughuli nyingi za kibiashara zinaendelea katika maeneo hayo.”ETDCO inaendelea na ujenzi na ukamilishaji wa line inayoelekea upande wa mpanda ambapo nayo inatarajiwa kuwashwa mwezi wa sita,”amesema.
Kwa upande wake Mhandisi wa Mradi wa Tabora -Katavi Kutoka Shirika la Umeme nchini (TANESCO)Mhandisi Daniel Runyamila amesema ni kwa mara ya kwanza gridi inaingia kwenye Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mlele ili wananchi wa maeneo hayo nao wanufaike na umeme.
Anesema mbali na wananchi kunufaika na umeme,hata upande wa kibiashara napo watu wataenda kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza kwa sababu kutakuwa na umeme wa uhakika na shirika kunufaika kujipatia kipato.”Tunawasihi wananchi kuwa mabalozi wazuri kwa ajili ya kulinda miundombinu ya shirika na hata kwa manufaa yao,”amesisitiza.
More Stories
Prof.Mbede:Nishati ya umeme wa Sola imepunguza vifo vya wajawazito
Rais Samia apongezwa kuanzisha bima ya afya kwa wote
Serikali yajipanga kudhibiti matumizi yasiyo sahihi kuelekea uchaguzi mkuu