Na Mwandishi wetu,Timesmajira
KAMPUNI ya Envaita nchini yaja na suluhisho la Kidigitali la kutumia njia mpya zakualika watu katika matukio mbalimbali badala ili kusaidia kuokoa muda ,kutunza mazingira na kupunguza usumbufu kwa waalikwaji.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuona hali ya ukuaji wa teknolojia duniani kuanza kukua kwa kasi na kuondokana na mifumo ya kinailojia na kuelekea katika mifumo ya Kidigitali.
Ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam,Meneja Mawasiliano wa Kampuni hiyo,PrayGod Mushi wakati akiongea na waandishi wa habari akitambulisha mfumo huo mpya wa utoaji wa kadi kwa njia ya kidigitali katika Mikutano mbalimbali iwe Harusi na Mikutano mikubwa inayofanywa na makampuni mbalimbali nchini.Amesema mialiko ya kidigitali inasaidia kwa kiasi kikubwa kupanga bajeti kwakuwa unakuwa na idadi kamili ya watu wanaohudhulia tukio lako.
“Kampuni yetu imeanza rasmi mwaka 2022 tukiwa na wafanyakazi wachache lakini kwa sasa tunawafanyakazi zaidi ya 30 ambapo tunafanya kazi nchi nzima kuhakikisha huduma ya kualika katika matukio mbalimbali kidigitali.

“Njia ya kidigitali ni nzuri lakini changamoto iliyopo watu bado hawaelewi wanadhani ni utapeli au wakati mwingine wanaona kama wanadharaulika kwa kutumiwa kadi za mialiko kwa simu lakini ndo teknoloji inavyotupeleka huko kwa sasa na kuondokana na mitazamo wa zamani,”amesema
Amesema kwa kutumia njia hiyo ya kidigitali wanahakikisha taarifa za ualikaji zote zinatakiwa kukaa katika mfumo huo na kujua ni walengwa gani wanapelekewa mialiko hiyo ambapo wao kazi yao nzima ni kuwasimamia kadi kufika kwa wakati kwa njia hiyo ya kidigitali na kufanya ufatiliaji wa kuwakumbusha kabda ya tukio.
“Mteja anapokuja kutupa kazi yake tunahakikisha tunaanza nae mwanzo wa utoaji wa kadi kwa njia hiyo ya kidigitali,kisha kuwatumia walengwa wake wote na sisi wenyewe tutaanza kuwakumbusha siku kabla ya tukio muhimu na siku ya tukio tunakuja wenyewe kusimamia watu wanapoingia kwa kuzihakiki (scan) kadi hizo ili kuzuia watu kuvamia,”amesema.
Amesema bado uelewa ni mdogo kwa watanzania wengi lakini kwa sasa taratibu wanaanza kuzoea kwa sababu kadi hizi zinawaondolea usumbufu wa ucheleweshaji wa utumaji wa kadi katika matukio yao.
“Mfumo wetu ulivyo kadi haiwezi kutumika mara mbili katika tukio wala hakuna atayeweza kuingia kwenye sherehe bila kualikwa hivyo mfumo unasoma maelezo ya mtu husika moja kwa moja pindi wanaposcan,”amesema
More Stories
Rais Samia ateua Wenyeviti bodi mbalimbali
Wazabuni Nyanda za Juu Kusini wanolewa matumizi ya Moduli
Vipaumbele vitano Ofisi ya Msajili wa Hazina 2025/26