January 5, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

EMIRATE yaongeza ufanisi katika huduma zake

Na Mwandishi wetu,timesmajira,Online

SHIRIKA la ndege la Emirates imesema itaendelea kuongeza  huduma zake kwa ufanisi hususani katika kushughulikia mahitaji ya wasafiri wake hasa katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Uviko-19.

Pia shirika hilo limesema linaendelea na mpango wake katika kushughulikia mahitaji ya wasafiri katika utunzaji na uhifadhiji wa mizigo yao unaendelea kuwa mzuri kwa kuhakikisha wateja wao wanakuwa huru na safari zao.

Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Emirates jana,ilisema shirika hilo linaendelea kuhakikisha linatoa huduma nzuri kwa wateja wao.

Aidha imesema shirika hilo linaendelea   kulinda  afya za wateja wao hususani katika kipindi hiki cha Uviko-19  katika kuhakikisha hali ya usalama inakuwepo katika kila hatua ya safari za abiria wake.

“Wasafiri bado watahitajika kupata chanjo kamili angalau siku 14 kabla ya tarehe ya kusafiri au kuwasilisha karatasi maalum waliyopima  COVID-19 ambayo uchukuliwa kati ya masaa 48 hadi 96 kabla ya kuwasili, kulingana na marudio,”imesema

Aidha taarifa hiyo imesema wakati nchi zinapunguza vikwazo vya kusafiri kwa watalii  hususani kwa watanzania ambao wamepata likizo ya mapumziko ya kwenda  katika nchi ya  Dubai, Uturuki, Maldives, Shelisheli na Urusi ambapo wameondoa hitaji la kuweka karantini wakati wa kuwasili kwa watu ambao sio wakaazi wan chi hizo.

Imesema Kila wiki shirika lao linatoa ndege za Emirates ambazo ni salama kwa abiria na zenye kuwabeba wateja mbalimbali ikiwemo familia.

“Wasafiri wamekuwa wakitafuta vitu vipya  vya kujifunza hivyo wakikaa ndani ya ndege za Emirate wanakuwa wapo huru katika kujifunza vitu vingi,”imesema