Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
ELON Musk ameanza tena upinzani wake dhidi ya mwanzilishi wa Microsoft, Bill Gates, huku akionya katika X (zamani Twitter) kwamba Gates huenda akakutana na changamoto za kifedha endapo Tesla itaipita Apple na kuwa kampuni yenye thamani kubwa zaidi duniani.
Kwa mujibu wa post ya mtandao wa Timesofindia.com, kauli ya Musk inahusishwa moja kwa moja na inayodaiwa kuwa hasara kubwa aliyopata Bill Gates ya $1.5 bilioni kutokana na kubeti dhidi ya hisa za kampuni ya Tesla anayomiliki Musk. Ingawa Tesla imepiga hatua kubwa, bado inashika nafasi ya pili nyuma ya kampuni ya Apple (wazalishaji wa Iphone na Mac) katika thamani ya soko, ikiwa inahitaji ukuaji wa karibu asilimia 200 ili kuchukua ya kwanza.
Katika posti yake kwenye X, Musk aliandika: “Ikiwa Tesla itakuwa kampuni yenye thamani kubwa zaidi duniani, kubeti dhidi ya Tesla itamfilisi hata Bill Gates.”
Bill Gates alikuwa mtu tajiri zaidi duniani kuanzia mwaka 1995 hadi 2010, na tena kuanzia 2013 hadi 2017. Kulingana na orodha ya mabilionea ya Forbes ya mwaka 2024, Bill Gates anashika nafasi ya 8 na thamani ya mali yake ikiwa $128 bilioni. Utajiri wake unatokana na vyanzo mbalimbali.
Nini maana ya beti ya ‘short position’?
Beti ya ‘short position’ ni mkakati wa soko la hisa ambapo mwekezaji anakopa hisa, anauza kwenye soko la wazi, kisha kuzirejesha baadaye kwa bei ya chini. Lengo ni kupata faida kutokana na kuporomoka kwa bei ya hisa.
Beti ya Bill Gates dhidi ya Tesla
Mivutano kati ya Elon Musk na Bill Gates inatokana na beti inayodaiwa kuwekwa na Gates dhidi ya hisa za Tesla. Katika mahojiano ya awali mwaka 2022, Gates alidai kwamba alifanya beti dhidi ya Tesla. Hata hivyo imedaiwa kuwa beti hii ilimletea Gates hasara ya $1.5 bilioni.
Hata hivyo kati ya wachangiaji mbalimbali katika posti za X, mchangiaji mmoja aliyejulikana kama Teslaconomics alichangia kwenye post ya CEO wa Tesla kwa kuandika: “Kubeti dhidi ya Tesla, kama alivyofanya Gates, kunaleta faida kubwa tu ikiwa kampuni inafilisika!
Bill Gates aliweka beti kubwa kwamba Tesla ingetoweka wakati kampuni yetu ilikuwa katika moja ya hali dhaifu miaka kadhaa iliyopita. Beti kubwa kama hiyo pia inasukuma bei ya hisa kushuka kwa wawekezaji wa kila siku.”
Aliongeza kusema, “Kwa kadiri ninavyofahamu, Gates bado ana beti kubwa dhidi ya Tesla mezani. Mtu anapaswa kumuliza kama bado ana hiyo beti. Ukosefu wa ufahamu wa nafsi na unafiki wa Gates ambaye alijitokeza kuniomba niachie michango kwa sababu zake za kimazingira ambazo kwa sehemu ni za kivumbi, huku akijaribu kupata $500M kutokana na kuanguka kwa Tesla.”
Akishiriki tena tweet hiyo, mtumiaji huyo alisema: “Hii ndiyo sababu ni ‘kivuli kikubwa’ kwa Bill Gates tangu siku ya kwanza $TSLA.”
Kwa wale wasiojua, mwaka huu, hisa za Tesla zimepanda kwa asilimia 56.91% kutokana na ushindi wa Rais mteule Donald Trump katika uchaguzi wa 2024 na uhusiano wa karibu wa Elon Musk na Trump.
Hisa za Tesla zilipanda hadi kiwango cha juu cha $400 baada ya Goldman Sachs kuongeza lengo la bei.
More Stories
Kambi ya wanasheria Katavi kuwajengea uwezo wananchi
Serikali yaimarisha uchumi wa kidigitali kukuza biashara mitandaoni
RAS Tanga aipongeza Lushoto DC kuvuka lengo mapato ya ndani