December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Elimu juu ya umuhimu wa taarifa binafsi za Afya yashika kasi

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

TAASISI ya Agrithamani imezindua kikundi cha waandishi wa habari za afya kidijitali nchini na kuwapiga msasa juu ya kuelimishe umma kuhusu umuhimu wa kulinda taarifa binafsi za afya na kuchagiza maboresho ya kisera na kisheria.

Kikundi cha wanahabari 15 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wanaotoka mikoa tofauti tofauti katika kuhakikisha kinafanya kazi zake bila changamoto yoyote ile kimefanikiwa kufika kwenye wizara ya Afya na kupata baraka zote kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kwa niaba ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amempongeza Mkurugenzi wa taasisi ya Agrithamani Neema Lugangira (MB) kwa kuwakutanisha baadhi ya waandishi wa habari kutoka sehemu tofauti tofauti nchini kwa lengo la kuhakikisha wanaelimisha jamii juu ya taarifa mbalimbali binafsi za Afya.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikundi hicho uliyoatanguliwa na semina maalumu kwa wahariri Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Neema Lugangira, amesema suala la ulinzi wa taarifa binafsi za wananchi bado ni changamoto, huku baadhi ya watu wanaokwenda hosptali kudai taarifa zao muda mrefu baada ya kutibiwa huwa hawapatiwi badala yake wanakutana na vikwazo mbalimbali.

Lugangira ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa CCM, anayewakilisha asasi za kiraia, amesema ni wajibu wa waandishi wa habari kuanza kuelimisha jamii na kupaza sauti kuhusu umuhimu wa taarifa hizo.

Naye Meneja Kampeni wa Taasisi ya Transform Health Beatrice Okechi, amesema takwimu za afya nimuhimu kwa kila mwananchi awe nazo na kila hosptali ina wajibu wa kuzitunza na kuzilinda.