Viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS wamekutana hii leo kujadili mapinduzi ya kijeshi nchini Mali, yaliyomuondoa madarakani rais Ibrahim Boubacar Keita.Â
Ni Kwa muda mrefu jumuiya hiyo imekuwa ikijaribu kusuluhisha mgogoro huo kabla ya mapinduzi ya Jumanne wiki hii.Â
Akizungumza Afisa wa jeshi la nchi hiyo  kanali Assimi Goita ametangaza jana kuwa ndiye kiongozi wa mapinduzi nchini humo.
Umoja wa Afrika tayari umeisimamisha Mali kufuatia mapinduzi ya Jumanne, na kuungana na jumuiya nyingine za kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa na ule wa Ulaya kulaani vikali mapinduzi hayo.
Kundi la mataifa matano ya kanda ya Sahel limewataka wanajeshi walioongoza mapinduzi kumuachia rais Keita na maafisa wengine wa serikali yake wanaowashikilia.
More Stories
Jafo aipongeza iTrust Finance kudhamini Soko la Jiba Souk
Viongozi CHADEMA, Odinga wakutana, wajadili hali ya kisiasa nchini
Utafiti na Teknolojia matibabu ya magonjwa adimu wasisitizwa