January 26, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ebitoke: Nilijiona sifai kugombea Umiss

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa vichekesho hapa nchini Anastazia Exavery maarufu kama ‘Ebitoke’ amesema, alijiangalia na kijitathmini kuwa hawezi kugombea Umiss kwa kile anachodai kimo chake hakimruhusu.

Ebitoke alitangaza kugombea kushiriki shindano la Miss Tanzania 2020, lakini msanii huyo amefunguka na kusema shindano hilo lilimshinda kwani alijiangalia kwenye kioo akasema kwa ufupi alionao asingeweza kushinda.

Akizungumza na eNewz ya East Africa TV inayoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12:00 Jioni, Ebitoke amesema, Umiss una vigezo vingi ukiwemo urefu lakini yeye sifa hizo alikuwa hana jambo ambalo lilimshinda.

“U-Miss ulinishinda kwa sababu nilijiangalia kwenye kioo mara nyingi nikasema na ufupi huu nitaenda kuwa miss gani ‘high hills’ zenyewe kutembelea shida, kiukweli nina kasura fulani hivi ila umiss ulinishinda na sio fani yangu” amesema Ebitoke.

%%%%%%%%%%%%%%