Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
DOYO Hassan Doyo amekuwa mgombea wa tano kuchukua fomu katika Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Mgombea Mwenza Chausiku Khatibu Mohamed kupitia Chama Cha National League For Democracy(NLD).
Doyo amechukua fomu hiyo jijini hapa leo Agosti 10,2025 huku akitaja sababu zilizomsukuma kugombea nafasi hiyo ambapo amesema kuwa sababu ni haki yake ya msingi ya kikatiba kwa mujibu wa sheria za nchi.

“Katiba inaniruhusu kupiga kura au kupigiwa kura kwahiyo mimi nimechagua kupigiwa kura kundi la kupigiwa kura kwa mujibu wa sheria za nchi.
“Lakini pili kuna mambo ambayo tunaona hayajakaa sawa,watanzania wanamaisha magumu hali ya afya zao siyo nzuri,matibabu ni ya wasisi sana,bima ya afya bado haijawa mwarobaini wa kuhakikisha watanzania wanaishi maisha mazuri lakini pia suala la ajira ni suala zito ambalo katika nchi yetu limekuwa ni shida.
Ameeleza Tafiti mbalimbali zinaonesha kwamba nguvu kazi inayomaliza Vyuo vya Kati inakaa mtaani zaidi ya miaka mitatu hadi mitano bila kupata chochote cha kufanya.
“Sasa nagombea nafasi hii ya Rais nikawe maamuzi ya mwisho katika sera niweze kushughulikia matatizo ya ajira.
“Watu watajiuliza kwanini nimeanza suala la ajira ni kwamba hapa tulipo wote hakuna ambaye hajaguswa kifamilia kuhusu suala la ajira katika familia.
Kwahiyo tukaona tukishughulika na suala la ajira ipasavyo maana yake tunakwenda kuwagusa watanzania wote bila kubagua mtu hata mmoja .

Hata hivyo mgombea huyo alifika katika Ofisi za Tume kwa kutumia Bajaji kwa lengo la kuunga mkono vijana wanaojishughulisha na kusafirisha abiria kwa usafiri huo.
“Mimi nimekuja na bajaji kwasababu ya kuunga mkono vijana wengi ambao wanajishuhulisha na maisha ya kawaida katika kusafirisha abiria kwa maana gani,Bajaji ndiyo kimekuwa chombo cha usafiri rahisi sasa kwa watanzania kwahiyo nimeona niwasapoti kuwapa moyo ili waone Rais ajae ndiyo jicho lake hili.
“Mimi nikiingia madarakani gari lolote la serikali lililonunuliwa zaidi ya milioni 200 inauzwa,tutafanya mnada tunanunua gari ya kawaida.TDI zile Land-rover mil.30,40 unazigiza unawapa Mawaziri wanaenda mikoani kufanyakazi yale mashangingi ya milioni 300,400,500 nikiwa Rais siwezi kutumia yale katika Serikali yangu itabana matumizi ili fedha tuipeleke kwenye miradi kwasababu miradi mingi inakwama kwasababu ya fedha.
Amesema kuwa ataendelea kutumia usafiri wa hali ya chini kuwafikia Watanzania.



More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi