September 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dotto Magari awataka CHADEMA kumuunga mkono Rais Samia

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mfanyabiashara maarufu wa Magari Tanzania Dotto Keto maarufu ‘Dotto Magari’ mepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha nchi inakua na amani hivyo amewataka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuacha siasa za uongo na kumpa Rais Samia kongole kwa kazi kubwa anayoifanya.

Magari amesema ;” Nyinyi majirani zetu mlikua hamna ofisi
Kwa takribani miaka 30, leo mama kajitahidi katoa fungu kawahamishieni ofisi na kupelekwa mikocheni mnataka nini majirani? “

Aidha Magari amewataka CHADEMA kumuunga mkono Rais Samia
kwa kutengeneza mazingira bora ya kuvutia wawekezaji na ya kufanyia biashara nchini.

“Mnasema nchi haina amani, ni amani gani mnayoitaka? Wawekezaji wamerudi, watu wanafanya wanachotaka,hata nyie mnaongea mnachojisikia, hiyo siyo amani? . Mama anafanya kazi kubwa, ameshughulikia umeme, maji, treni ya umeme, barabara kujengwa kwa viwango na viwanda, mpeni Rais Samia maua yake kwani anafanya mengi kwenye hii nchi”

“Mkikaa kwenye vikao vyenu kuweni wakweli kwamba mama samia ndiyo kila kitu, apewe mitano yake na akija tena apewe mitano mingine jumla 10, huyu mama ndiyo aliyeweza kuiongoza hii nchi” Amesisitiza