January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ATLANTA, GA - SEPTEMBER 08: DMX performs at the 10th Annual ONE Musicfest at Centennial Olympic Park on September 8, 2019 in Atlanta, Georgia.(Photo by Prince Williams/Wireimage)

DMX kuzikwa April 25

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MAZISHI ya msanii maarufu wa muziki wa Rap nchini Marekani na mwigizaji DMX, yanatarijiwa kufanyika April 25 mwaka huu, ambayo pia yatakua mazishi ya faragha kwa maana yatakuwa ya familia na marafiki wa karibu wa msanii huyo watakaohudhuria.

Kwa mujibu wa aliyekuwa Meneja wa Rapper huyo amesema, zoezi la watu wote kuaga mwili wa Marehemu utafanyika April 24, katika Ukumbi wa Barclays Center huko Brooklyn nchini Marekani.

DMX aliaga dunia hivi karibuni alipolazwa katika hospitali moja baada ya kupata matatizo ya mshtuko wa moyo wiki iliyopita. Hali ya afya ya msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Earl Simmons, ilizidi kuwa mbaya ndani ya wiki 1 na akaanza maisha ya kutegemea mimea ya asili.

Hata hivyo, familia yake ilitangaza kuwa mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 50 alifariki. Albamu za mwimbaji huyo ziliuzwa kwa mamilioni kote ulimwenguni. Mbali na hivyo, pia DMX aliwahi kuigiza katika filamu ya Romeo Must Die.