April 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt,Mandai na Murtaza washiriki mbio za hisani za Bunge

Na Heri Shaaban

Mjumbe wa Baraza la Wazazi Taifa Dkt.Ally Mandai na Mbunge wa Viti Maalumu, Najma Murtaza,wameshiriki mbio za hisani kwa ajili kuchangia fedha za ujenzi wa shule ya Bunge Wavulana iliopo mkoani Dodoma.

Ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewakikishia, watanzania fedha zilizokusanywa katika mbio za hisani zinaenda kutumika zilivyokusudiwa katika kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya sekondari Bunge Wavulana.

Huku akisema,shule hiyo ya kidato cha tano na sita itajengwa katika eneo la Kikombo jijini Dodoma karibu na shule ya Wasichana iliyojengwa na Wabunge wanawake mwaka 2020.

Akizungumza mara baada kumaliza mbio za hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za ujenzi wa shule ya Bunge Wavulana ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Dkt. Mandai amesema,Jumuiya hiyo ipo mstari wa mbele kuisaidia Serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo ya afya,elimu na utunzaji mazingira.

Mbunge wa Viti maalumu, Najma Murtaza alipongeza Serikali katika kukuza sekta ya michezo na elimu.