Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. Jim Yonazi ameongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi ngazi ya Makatibu Wakuu kilicholenga kupitia utekelezaji wa maboresho ya rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia 2033 na rasimu ya Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia 2033 yaliyotolewa na Waziri Mkuu wiki moja iliyopita Machi 23, 2023 Mkoani Dodoma.
Dkt.Yonazi ameongoza Kikao hicho kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ngazi ya Makatibu Wakuu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi.
Kikao hicho kimehusisha Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka na Wajumbe wa Kikundi Kazi cha Taifa cha Nishati Safi ya Kupikia kilichofanyika Machi 30, 2023 Jijini Dodoma.
Dkt. Yonaz amesema kuwa kikao hicho ni mahsusi kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa maboresho na maelekezo yaliotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipokutana na Mawaziri na Naibu Mawaziri Machi 23, 2023 Mkoani Dodoma.
Mara baada ya Makatibu Wakuu hao kupitia Rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi safi ya Nishati Safi ya Kupikia 2033 na Rasimu ya Mpango Mkakati wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia, itawasilisha kwa Waziri Mkuu tarehe 31 Machi 2023.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi