January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Yonanzi akutana na uongozi wa TECDEN

Na Mwandishi wetu.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Taasisi ya Tanzania ECD Network (TECDEN) Jijini Dodoma.

Dkt. Yonazi amekutana na uongozi huo Mei 7, 2024 ambapo walijadili kuhusu kazi za Taasisi hiyo ikiwemo ya uratibu wa Mashirika na Wadau wasio wa Kiserikali katika masuala mazima ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto wadogo kuanzia umri 0 hadi miaka 8.

Katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa Serikali  itaendelea kushirikiana na Wadau ikiwemo Taasisi hiyo ili kuendelea kuleta matokeo yenye tija kwa Taifa.