Na Esther Macha , Timesmajira Online, Mbeya
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Spika wa Bunge,Dkt Tulia Ackson,Novemba 12,2024,amewakabidhi nyumba wahitaji watatu wanaoishi katika mazingira magumu Kata za Iyunga mtaa wa Inyala na kata ya Ilemi jijini humo.
Ambapo katika kumuunga mkono Dkt.Tulia Wabunge wa Jimbo la Mbarali Bahati Ndingo na Mbunge wa Jimbo la Rungwe,Mwantona walikabidhi kiasi cha shilingi 600,000 kwa wahitaji hao.
Huku Mbunge wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya Bahati Ndingo,amesema Dkt.Tulia, amewezesha kiuchumi wananchi wa Jimbo hilo wakiwemo vijana,wanawake na wazee.Ambapo ni kiongozi wa mfano anayepaswa kuheshimiwa na kulindwa.
“Hakuna kundi ambalo Dkt.Tulia ameliacha katika uwezeshaji wananchi kiuchumi,ikiwemo kuwezesha vijana pikipiki 100, na wengine kiuchumi,wazee bima za afya, wanawake wamewezeshwa mikopo ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji.Hata kwangu Mbarali ameweza kusaidia ingawa siyo Jimbo lake,”amesema.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rungwe,Antony Mwantona amesema kwa umoja wao wataendelea kumuunga mkono Dkt.Tulia kwani licha ya kusaidia makundi mbalimbali jijini hapa,bado amekuwa akisaidia hata wananchi wasiokuwa wa Jimbo la Mbeya Mjini hivyo anapaswa kulindwa kwa nguvu zote.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote