November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Tulia wanaume msikimbie wake zenu wanapozaa watoto wenye ulemavu

Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya

SPIKA wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt.Tulia Ackson amewataka wanaume kutowakimbia wake zao pindi wanapojifungua watoto wenye ulemavu badala yake wakae kwa pamoja katika kutafuta Suluhu iliyotokea.

Dkt. Tulia amesema hayo leo wakati akifungua zoezi la uchunguzi wa awali wa huduma ya matibabu ya macho bure inayotolewa kwa siku tatu na Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Tulia Trust na Beta Charitable Trust ya nchini Uingereza.

Dk Tulia amesema kuwa kumekuwa pls na tabia ya baadhi ya wanaume kutekeleza familia zao pindi wanapobaini wake zao kujifungua watoto wenye ulemavu.

Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Tanzania, Ain Sherif akitoa maelezo ya huduma hiyo kwa Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson

“Wanaume mnapopata watoto wenye ulemavu ni jukumu lenu kuwatunza na kuwafikisha kupata huduma za matibabu kwa madaktari bingwa kwani kuna Matatizo ambayo haya kosi tiba” amesema.

Ameongeza kuwa wanaume msiwakimbie akina mama mnapokuwa mmepata watoto wenye changamoto chukueni hatua kwa mtoto aliyepata changamoto kama ambavyo mnakuwa pamoja katika kutafuta mtoto “amesema.

Aidha Dkt.Tulia amesema hayo kufuatia mtoto mdogo aliyepimwa na kubainika na changamoto ya Uoni aliletwa na wazazi wake wote wawili jambo lililomshangaza Spika kwani wanaume walio wengi huwatelekeleza wake zao wanaojifungua watoto wenye ulemavu.

Kwa upande wa wananchi waliofika kupata matibabu ya macho wamesema kuwa wanaiona Mbeya mpya kwa jambo kubwa alilofanya Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini la kuleta taasisi hiyo ili isaidie wananchi kupata matibabu ya macho.

“Mimi ni mmoja wa wananchi niliyefika hapa kutoka kata ya forest kupata huduma hii nimeteseka kwa muda mrefu na tatizo hili la macho lakini sasa nimefanyiwa upasuaji nipo vizur nasema Mbunge wetu abarikiwe maana hata wananchi tusio na uwezo tumepata tiba bure kabisa “Amesema Daudi Johana mkazi wa forest.