December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Tulia awasili Vienna nchini Austria kushiriki mkutano wa kimataifa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

RAIS wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mei 19 i, 2024 amewasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Austria na kupokelewa na Mwenyeji wake Mhe. Naimi S. H. Aziz, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna.

Dkt. Tulia yupo Vienna nchini Austria, ambapo anatarajia kushiriki Mkutano wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Nyuklia (ICONS-2024) utakaofanyika kuanzia kesho tarehe 20-24 Mei, 2024 akiwakilisha IPU kwenye Mkutano huo.