Na Esther Macha,TimesMajira,Online,Mbeya
MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson ametoa mkopo wa Bodaboda tano zenye thamani ya shilingi milioni .12 kwa kikundi cha vijana Iziwa.
Dkt Tulia amesema yeye kama Mbunge lengo lake ni kuhakikisha anawawezesha vijana waweze kujiajiri wenyewe na kuendesha maisha yao.
Aidha Mbunge huyo amesema kuwa wanawake nao ni muhimu wakajiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa mikopo ambayo itawawezesha kuendesha maisha yao.
Akizungumzia kuhusu bima ya afya Dkt Tulia amewataka wananchi kukata bima za afya ni jambo zuri ambalo linaweza kuwasaidia pale wanapoumwa na kusema kwamba kuna CHF iliyoboreshwa hivyo wana nafasi ya kujiunga.
Kwa upande wake Rais wa bodaboda Jiji la Mbeya, Aliko Fwanda amesema siasa zimeisha sasa wanachapa kazi.
Naye Mwenyekiti wa Bodaboda Iziwa ,Zuberi Ndidi wameshukuru kwa mkopo huo na kuhakikisha watajituma kufanya kazi na kuwa mfano kwa wengine.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili