Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
TAASISI ya Tulia Trust inayoongozwa na Mkurugenzi wake Dkt.Tulia Ackson ambaye pia ni Spika Bunge imetimiza ahadi yake ya kuwasomesha watoto wawili waliokuwa wakiishi mazingira magumu na hivyo kushindwa kuendelea na masomo kutokana na hali ya kimaisha iliyokuwepo katika familia hiyo.
Kauli hiyo imetolewa Julai 24,2025 na Meneja wa Taasisi ya Tulia Trust,Jackline Boaz mara baada ya kuwakabidhi watoto wawili wa familia ya Kapangala shule ya sekondari Uwata na mwingine shule ya msingi Uwata ambapo gharama za masomo zote zitagharamiwa na Tulia Trust ambayo ipo chini ya Mkurugenzi wake Dkt.Tulia Ackson .
Boaz amesema kama Taasisi wameamua kuwachukua Watoto na kuwaendeleza na elimu kutikana na hali ya kimaisha waliyonayo familia hiyo ya kushindwa kumudu grama za kusoma Boaz.
“Gharama zote tulizotumia ni zaidi ya Mil.5 na kuanzia sasa Hawa watoto watakuwa chini ya Taasisi yetu kwa kila kitu na hata kipindi cha likizo watakuwa chini ya Taasisi hii kwa mahitaji yote ya shule na mahitaji mengine muhimu “amesema.
Watoto hao ni Nature Nenelo (18), aliyefaulu kidato cha nne kwa daraja la kwanza na alama 13 na kushindwa kujiunga na elimu ya juu kutokana na ukosefu wa karo ambapo sasa Nature amepelekwa Shule ya Sekondari UWATA kuendelea na masomo ya kidato cha tano huku mdogo wake Patrick Nenelo (8) aliyekuwa akisoma darasa la kwanza Shule ya Msingi Mwasote amehamishiwa Shule ya Msingi UWATA
Akizungumza baada ya kuwakabidhi shuleni hapo Meneja wa taasisi ya Tulia Trust Jackline Boaz amesema taasisi hiyo imeamua kuwasaidia watoto hao kama sehemu ya juhudi za kusaidia watoto wenye ndoto za kielimu zisikome kutokana na hali ngumu ya maisha huku akisema kiasi cha shilingi milioni tano na laki nane (5,800,000/=) kimetumika kugharamia mahitaji ya watoto hao.
“Tumechukua kumwendeleza kijana huyu kutokana na Maisha duni kwenye familia yake kwani ametoka kwenye familia ambayo haijiwezi kujikidhi kuweza kumsaidia kupata elimu,pia yupo Mdogo wake nae anaenda kuanza masomo yake shule ya msingi Uwata kwetu sisi ni Kama baraka”amesema Meneja huyo.
Mtoto Neture amesema kuwa amemshukuru dkt.Tulia kutoa ahadi ya kuhakikisha anapambana pia amesema kitendo kilichofanywa na Dkt.Tulia cha kujali wenye uhitaji kimeipa faraja kubwa familia hiyo ambayo ilikuwa imekata tamaa na kusema licha ya kukata tamaa lakini bado aliendelea kuwa mtulivu .

Aidha Kijana huyo amesema kuwa ni jambo ambalo hakutegemea kama siku moja angekuja kusoma na kusema hawezi lumkatisha tamaa Dkt.Tulia, pia amesema familia aliyotoka ndoto zake za kusoma yeye na mdogo wake walikata tamaa ya kuendelea na Masomo.
Bibi wa watoto hao,Melisia Kapangala amesema kuwa watoto hao amelea kwa kupika pombe Lakini imefika wakati ameshindwa . mpaka kushindwa hata chakula hivyo Kwa msaada huu anamshukuru Dkt.Tulia.
“Nimelea kwa shida mpaka sasa hata chakula hapa ndani ni shida MUNGU amsaidie Dkt.Tulia hapa nimekwama Hawa watoto nimelea kwa kuhangaika kupika pombe na kufanya vibarua ili niweze kuwasomesha watoto Hawa maana mama wa watoto hana uwezo wowote “amesema Bibi wa watoto hao.
Kaimu Mkuu wa shule ya sekondari Uwata Boys Mwl.Lazaro Kilalawima amesema kuwa wameona mchango mkubwa kwa Taasisi ya Tulia Trust kwa jamii ambazo zinatoka kwenye mazingira magumu na kusema wapo vijana wengi ambao wanasomeshwa na Dktr.Tulia.
“Tumempokea kijana Necha ambaye anaanza kidato cha Tano Mimi niahidi kwamba stags ya vizuri sanaa kwasababu walimu wapo na jitihada za kumsaidia zipo wana mbinu mbali mbali,tumeona jitihada kubwa za Bunge kusaidia katika maeneo tofauti hasa eneo la elimu hivyo niombe wana Mbeya tumpe sapoti Dkt.Tulia ,tunao vijana wengine hapa wanasomeshwa na Dkt.Tulia wanafanya vizuri sanaa katika masomo yao”amesema Kaimu mkuu wa Shule.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Mwasote January Robert Kalumiana, ameishukuru taasisi ya Tulia Trust kwa moyo wa upendo na msaada huo wa kielimu huku Husna Mgoba, Mjumbe wa serikali ya mtaa huo akaeleza jinsi walivyoshirikiana na viongozi wengine kufanikisha maombi ya msaada huo kwa familia hiyo.
Kijana Nature alifaulu kidato cha Nne na kupata ufaulu wa A na kupangiwa Shule ya sekondari Rungwe lakini kutokana na Shule aliyopangiwa kutokuwa na Masomo yake uongozi wa Tulia Trust uliangalia shule nyingine na kupata Uwata Sekondari ambayo ni shule ya watoto wa kiume pekee ambayo ipo Mbeya mjini.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi