March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Tulia achukua fomu ya uteuzi Ubunge Jimbo la Uyole

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online-Mbeya

AlLIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson amechukua fomu ya uteuzi wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Uyole kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Dkt. Tulia amechukua fomu hiyo Agosti 25, 2025 na inayotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi(INEC),kupitia Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Uyole katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mbeya..

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo Dkt.Tulia,amesema CCM,imejipanga kuhakikisha kinapata ushindi kuanzia ngazi ya Udiwani ,Ubunge pamoja na Urais.

“Muda wa kampeni utakapofika ndugu zangu tupambane ili kura zimwagike pia Rais Samia lazima tumwambie asante kwa kutupa Jimbo jipya la Uyole,”amesema Dkt.Tulia.