Na Esther Macha Timesmajira Online,Mbeya
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt.Tulia Ackson amekabidhi mabati bando 11 na fedha kiasi cha milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Kata ya Itezi.
Dkt.Tulia ametoa vifaa hivyo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo kutokana na ombi la uongozi wa Kata hiyo ili iweze kusaidia shughuli za serikali.
Hata hivyo Dkt Tulia ameishukuru kamati ya ujenzi kwa kazi kubwa waliyofanya ya kusimamia ujenzi huo wa ofisi, amesema serikali ndio inajenga ofisi lakini wana Itezi wamefanya wenyewe hata kama serikali itakuja sawa na isipokuja bado ujenzi huo utaendelea.
“Niwashukuru sana kwa jitihada zenu katika kuchangia shughuli za maendeleo,nafahamu baadhi yenu hamtoi michango tu hapa Itezi bali mmekuwa mkijitoa nje ya hapa na tunawasikia,mnatudaisaidia sana katika kuhakikisha Jiji letu linapiga hatua kwenye maendeleo,nimeleta mchango wangu wa milioni 2 ili kuhakikisha jengo letu linafika hatua fulani,”amesema Dkt.Tulia.
Diwani wa Kata ya Itezi Sambwee Shitambala amemshukuru Spika kwa namna anavyoipambania Kata hiyo katika kuhakikisha shughuli za maendeleo zinasonga mbele ikiwemo ujenzi wa shule na mahitaji mengine muhimu kwa wananchi.
Katibu wa Kamati ya ujenzi wa ofisi hiyo Alex Kijombo,amesema kuwa kamati ilikutana na wana mtaa kupitia mkutano wa hadhara ulioitshwa na viongozi wa mtaa na kuwasilisha gharama za ujenzi huo.
Huku akieleza kuwa kukamilika kwa ofisi hiyo ya kisasa kutarahisisha utendaji kazi kwa viongozi wa Kata ya Itezi ambao walikuwa wakipanga.
More Stories
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake