Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Bagamoyo
MKURUGENZI Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware, amewataka watumishi wa baraza hilo kuwa na ushirikiano, kujitoa kwa wengine, kupendana, kuheshimiana ili kufikia malengo tarajiwa kwa mstakabali wa mazingira nchini.
Sware,ameyasema hayo Desemba 15, 2024,wakati akizungumza na watumishi wa NEMC nchini, katika hafla ya pamoja iliyofanyika eneo la Ndoto Pole Pole Farm lililopo Bagamoyo,iliyohusisha burudani mbalimbali na michezo chanya yenye kuleta na kuimarisha ushirikiano kazini na uhusiano mzuri katika kufikia malengo chanya.
“2024 ni mwaka wa NEMC kujitafuta na kujitathmini,kutengeneza njia inayotupasa kufikia malengo, na ndio maana nilitaka tujuane, tujengane na tuwekeane malengo, ambayo mwaka 2025 utakuwa ni mwaka wa kuyatimiza na kuchukua hatua,” amesema Dkt. Sware.
Pia, ameongeza kuwa NEMC kama chombo chenye dhamana ya kusimamia mazingira nchini, kinapaswa kusimamia dhana ya ushirikishwaji ili kufikia malengo, huku akisema kuwa, mazingira ni watu hivyo kuna umuhimu wa kuyaendea malengo chanya kwa wakati na weledi ili kuleta mafanikio chanya.
More Stories
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza
Rais Samia atimiza ahadi Hanang