June 2, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Samia:Wasio na uwezo msiwaonee haya

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaasa wanaCCM kutowaonea haya wagombea  wa nafasi mbalimbali za Uongozi kwenye mchujo wa kuwapatia wagombea watakaopeperusha bendera kupitia chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu ujao kwa kuchagua watu wenye sifa na uwezo wa kuleta maendeleo ya watu na Taifa kwa ujumla.

Dkt.Samia ameyasema hayo Leo Mei 30,2025 jijini Dodoma wakati akifunga Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho ulioanza Jana Mei 29,2025 na kuhitimishwa leo katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

 Pia alielekeza kuwa ifikapo Juni  1 mwezi ujao, awe amepokea majina ya wagombea Ili kuandaa Mafunzo kwa watu watakaochuja majina.

Aidha Rais Samia aliwataka wanachama na viongozi wote wa chama kuhakikisha kuwa baada ya uchaguzi, mshikamano huo unaendelea kuwepo bila migawanyiko. 

Alisisitiza kuwa chama kinahitaji watu wenye uadilifu na uwezo wa kutekeleza ilani kwa ufanisi, si wale wanaotafuta nafasi kwa malengo binafsi. 

Alisema, “Tusiwape watu nafasi kwa sababu tu ya ukaribu au umaarufu,tuwape wanaojua wajibu wao na wanaoweza kuwatumikia wananchi