Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Ruvuma
MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,Septemba 20, 2025 amefika katika uwanja wa Veta, uliopo maeneo ya Msamara mjini Songea, ili kukagua maendeleo ya maandalizi ya uwanja huo kwa ajili ya mkutano mkuu wa kampeni utakaofanyika Septemba 22, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameambatana na Mgombea Mwenza, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, amesema, maandalizi yote yanaendelea vizuri kwa ajili ya kumpokea Mgombea kiti cha Urais kupitia chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anayetarajiwa kuwasili kesho.

Mwenyekiti huyo amesema,Dkt.Samia anatarajiwa kuwasili Septemba 21, katika uwanja wa Ndege wa Songea, ambapo atapokelewa na Mgombea Mwenza, Dkt. Emmanuel Nchimbi, viongozi wa chama pamoja na wananchi wa Mkoa huo.
Ameeleza kuwa, ziara yake itaanzia katika Wilaya ya Nyasa, ikiwemo kusimama Mbinga, ambapo atazungumza na wananchi kisha kufanya mkutano wa kampeni katika eneo la Mbamba Bay.
Aidha, Septemba 22, 2025 imeelezwa. Dkt. Samia atafanya mkutano katika uwanja wa Veta, eneo la Msamara mjini Songea, kabla ya kuelekea Namtumbo na Tunduru, ambapo atafunga kampeni kwa Mkoa huo , huku Septemba 23, 2025 akitarajiwa kuanza kampeni mkoani Mtwara.


More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama