Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, leo Mei 29,2024 ametekeleza ahadi yake wilayani Manyoni kwa kutoa kiasi cha milioni 18 kwa ajili ya kuezeka jengo la kitega uchumi la ofisi ya CCM Wilaya hiyo.
Rais Samia ametekeleza ahadi hiyo leo kupitia Katibu Mkuu wa Chama hicho, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.

Katibu Mkuu huyo ametangaza hayo mbele ya Kamati ya Siasa ya Wilaya, Manyoni, akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Singida ikiwa imeanza leo na kutarajiwa kumalizika kesho.
Amesema hiyo ilikuwa ni ahadi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa kupitia kwa Katibu Mkuu wa zamani Daniel Chongolo.

More Stories
Fedha za Mfuko wa Jimbo ziingizwe kwenye mfumo wa NeST
Dkt.Biteko awataka wanawake kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia
Biteko: Afrika tunayapa kipaumbele matumizi Nishati Safi kukabiliana mabadiliko ya Tabia nchi