March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Nchimbi awasili Mwanza kwa ajili ya kampeni

MNa Agnes Alcardo,Timesmajira Online-Mwanza

MGOMBEA mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,leo Agosti 29,2025,amewasili ,jijini Mwanza kwa ajili ya kuzindua kampeni Mkoa wa Mwanza kuelekea katika uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 29,mwaka huu.

Balozi Nchimbi, amewasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza na kupokelewa na viongozi wa chama hicho na wananchi wa Mwanza, ambapo baadae ataelekea wilayani Keimba kwa ajili ya mkutano mdogo.

Kisha Misungwi na Buhongwa wilayani Nyamagana atasalimiana na wananchi na baadaea atakuwa na mkutano mkuu wa kufungua kampeni utakaofanyika uwanja sa Furahisha wilayani Ilemela.