Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amewasili mkoani Arusha leo, Septemba 12, 2025 kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni akitokea Mkoa wa Katavi.
Mara baada ya kuwasili jijini humo, Balozi Dkt.Nchimbi ataelekea Wilayani Longido katika Jimbo la Longido, ambako atawahutubia Wananchi wa jimbo hilo na kuwanadi Wagombea Ubunge wa majimbo ya Mkoa huo, akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Longido ,Dkt Steven Kiruswa pamoja na Madiwani.

Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo.

Aidha, amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.


More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI