Na Penina Malundo,Timesmajira
CHAMA cha Mapinduzi (CCM)kimechangia Milioni 10 ya ujenzi wa Ofisi ya Chama Jimbo la Mtwara Vijijini huku likisisitiza kuendelea na utekelezaji wa ilani zake katika jimbo hilo licha la kuwa la Upinzani.
Akizungumza leo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi na Mtwara leo tarehe 29 Julai 2024 ,wakati akisalimiana na kuzungumza na Wananchi wa Jimbo la Mtwara Vijijini Kata ya Mpapura ambalo liko Upinzani.
Amesema pamoja na kwamba jimbo hilo liko upinzani lakini utekelezaji wa Ilani katika jimbo hilo upo wa kiwango cha juu.
“Katika jimbo hili tumemuweka Kaimu Mbunge Chikota anaefanya shughuli hapa hakika kazi imefanyika nafikiri mmeona sasa kazi kwenu wakati ukifika inabidi mbadilike kwani mnapata maendeleo lakini hamna wa kumhoji,”amesema.
Aidha amesema CCM inawfanya mambo makubwa katika kutekeleza ilani yake hivyon wakati ukifika pigeni chini wasiobadilika kichagueni Chama cha Mapinduzi.
Dkt.Nchimbi amewaasa Wananchi na wanaccm wa Mpapura kuendelea kutunza na kulinda amani na utulivu wa nchi ba asitokee Mtu akawadanganya watu kuhusu kuharibu amani iliyonayo
Katibu Mkuu wa CCM ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa-NEC, Oganaizesheni, Issa Usi Haji Gavu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA- Amos Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa-SUKI- Rabia Hamid Abdalla katika ziara hiyo huku wakiwa wamemaliza ziara yao mkoani Mtwara na kuanza rasmi mkoani Lindi leo.
More Stories
Waziri Mavunde awakaribisha wawekezaji wa madini kutoka Finland
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar azindua kampeni Katavi
Waziri Nchemba mgeni rasmi mahafali ya 17 ITA