December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Nchimbi apokea taarifa utekelezaji wa Ilani ya CCM,Jimbo la Mchinga

Na Penina Malundo,Timesmajira

KATIBUĀ  Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi apokea taarifa ya utekelezaji wa ilani Jimbo la Mchinga na kumpongeza Mbunge wa Jimbo kwa kutatua kero za wananchi wake.

Ameyasema hayo leo jimbo la Mchinga Mkoani Lindi wakati wa upokeaji wa taatifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 – 2025,Dkt.Nchimbi amesemaĀ  tayari Mbunge wa Jimbo hilo ,Salma Kikwete ametembeleaĀ  kata zote na vijiji vyote.

” Umetumia hadi bodaboda na bajaji kuwafikia wananchi wa Jimbo la Mchinga, unaguswa na changamoto za wananchi wenzako wa Mchinga na unapambana kutatua kero zao kwa kuzisemea bungeni na kuwaomba mawaziri kufika huku wao wenyewe.

“KwaĀ  Ā niaba ya CCM nakupongeza wewe na viongozi wenzako kwa kazi kubwa unayofanya..wakatiĀ  natazama ile video ya uwasilishaji wa taarifa hii ya utekelezaji wa ilani, kuna mama mmoja amesema hakutegemea kwa hadhi yako ulivyo, kwamba ungeweza kulizunguka jimbo zima la Mchinga,”amesema.

Amesema yeye pamoja naĀ  wenzakeĀ  Wajumbe wa sekretarieti wamefurahishwa na utekelezaji huo mzuri wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi 2020/2025, ndani ya miaka hii mitatu.Ā 

Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Salma Kikwete wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/2025,amesemaĀ kwa kipindi kifupi cha miaka mitatu ya ubunge wake jimbo la mchinga limebadilikaĀ  ukilinganisha na hali ilivyokuwa kwa mwaka 2020 .

Amesema katika ilani ya ccm ya mwaka 2020 hadi 2025,Chama kimesisitiza umuhimu waĀ  huduma za jamii na kuahidi kuziboresha ili kumfanya kila mwananchi kupata huduma bora na kwa wakati.

“Huduma za jamii zilizoainishwa ni pamoja na Elimu,Afya,Maji,Miundombinu na nyinginezo ,”amesema na kuongezaĀ 

“Katika jimbo letu la mchinga tumepata manufaa makubwa katika sekta hizo na baadhi ya mafanikio hayo kisekta ni sekta ya ElimuĀ  ambapo walifanikiwa kupata kiasi cha Bilioni 18.4 fedha ambazo ni nyingi ikilinganishwa na miaka ya nyuma fedha zilipangiwa matumizi mbalimbali,”amesema.

Aidha amesemaĀ  zaidi ya vyumba vya madarasa 300 vimeongezwa ndani ya miaka mitatu ambapo madarasa ya awali 79,madarasa ya shule ya msingi 591 na madarasa ya sekondari 282.

Mbunge Salma amesema katika sekta ya maji huduma ya maji katika jimbo lao inapatikana kwa asilimia 80 ndani ya miaka mitatu.

“Katika Sekta ya afya zaidi ya Bilioni 4.83 zimepokelewaĀ  kwaajili ya miundombinu na vifaa vya afya ,vifaa tiba,Afya ya Msingi na Chanjo pia tunashukuru kutuongezea watumishi wa afya maana wakati tunaingia madarakani jimbo lilikuwa linawatumishi wachache sana wa afya.

“Miundombinu ya barabara kipindi cha miaka mitano barabara hizi zimekuwa zikifanyiwa matengenexo mbalimbali kwa kutumia vyanzo vinne vya fedha ambavyo ni mfuko wa Jimbo,Tozo ya Mafuta na Fedha maalum ambapo kazi zilizofanyika ni ujenzi wa madarasa 2 katika barabara ya Milola -Nangaru na Mipingo -Mnyangara,madaraja kati ya 4 katika barabara ya Chikonji -Nangaru,Moka-Mtumbukile na Nangaru -Milola.Pia makaravati 25,madaraha ya waya 2 katika barabara ya Mchinga-Sinde na Mchinga -kijiweni.Zege za mstari mita 320katika barabara ya chikonji -Nangaruna Mlola-Kiwawana Zege barabara mita 200 katika barabara ya Milola na Namtamba,”amesema .

Akielezea sekta nyingine,Salma amesema katika sekta ya Nishati- jimbo lao ni miongoni mwa majimbo yaliyofaidika na mradi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA ).

“Wakati naingia jimboni mradi wa REA ulikuwapo lakini ulikuwa na changamoto ikiwamo wananchi kupitishiwa na nguzo bila kuwekewa umeme na baadhi ya maeneo umeme kutolewa kwa upendeleo,”amesema.

Ā 

Amesema sekta nyingine zilizotekelezwa niĀ  Sekta ya uvuvi,mifugo,Kilimo,Maliasili na Utalii ,mikopo ya vijana wanawake n watu wenye wenye ulemavu,Kuendele,a michezo ,ushirikiano katika shughuli za chama na jumuiya.Ā