January 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vitendo vya kuchukua sheria mkononi vilaaniwe

Na Penina Malundo,Timesmajira

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa rai kwa watanzania kulaani vitendo vya kujichukulia sheria mkononi huku akiwaasa kutoa fursa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya majukumu yao.

Akizungumza hayo leo ijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Amani Simbayao ambaye ni miongoni mwa maofisa watatu walioshambuliwa na wananchi Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es Salaam wakati akitaka kukamata gari linalodaiwa kuingizwa nchini kimagendo.

Nchemba amesema ni jambo baya pamoja na kwamba binadamu yeyote njia yetu ni moja ya kuonja umauti ila kwa hili ni njia ya kulazimisha.

“Ni jambo baya kwa sababu yeyote ile ni jambo ambalo halikubaliki hapa nchini poleni sana wafiwa wote,hili ni jambo linalopaswa kulaaniwa na Mtanzania yeyote ,mpenda mema wa nchi yetu,”amesema.

Amesema TRA imekuwa ikifanya vizuri ndani ya miaka mitatu hadi sita,tangu itii maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.”Mmejitahidi sana kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Rais Samia kukusanya kodi kwa weledi na kuzingatia Sheria mmejitahidi.

Kwa upande wake wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,CPA Amos Makalla ametoa rai ya namna bora ya kutunza familia ya Amani ili watoto wake wasome katika mazingira mzuri.

”Kwa sisi watumishi waTRA wa nchi nzima tukitoa shilingi 10,000 tu tukaenda tukanunua bondi pale BOT watoto wakapata mshahara …pesa hizo zitajenga kujiamini kwa watoto hawa , tukifanya hivi tutaepusha migogoro inayotokana na mirathi”,alisema Charamila

Alisema kuwa kuuawa kwa Amani kumelitia hasara Taifa ambayo  haina mbadala.”Hatuwezi kusema amani atapata mbadala kwenye dunia hii tushapigwa hasara kubwa sna ka taifa na familia yake.

“Amani amefungua ukurasa mpya kwenye utawala wangu kama Mkuu wa MKoa na lazima huu ukarasa lazima ujibu na lazima ulete mashahidi.. lazima damu iliyomwagika itabeba lazima eneo lilitokea tukio patasafishwa na nikisema patasafishwa patasafishwaje , sijawahi kuwa kiongozi legelege kwenye mambo ya msingi siku zote nabeba maamuzi mazito,”amesisitiza 

Awali akitoa salamu za pole Kamshna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda akito amesema kuwa watumishi wa TRA ambao ni kikosi cha ukusanyaji kodi ya ‘Fast’ kitapewa ulinzi wa jeshi la polisi ili kuhakikisha usalama wao .

“Kama ambavyo tumekubaliana kuwa hatutatumia nguvu kwenye kusimamia kodi tutaendelea hivyo lakini kwa kile kitengo cha ‘Fast’ ambacho kinapambana na walioamua kukwepa kodi kuanzia sasa hatutawaacha wafanyakazi pekee yao watafanya wakiwa na Polisi”.

Amesema Marehemu Amani amefariki lakini amefariki kwa sababu ya kushambuliwa lililotokea wakati anatimiza majukumu yake ya kuisaidia nchi hii na wananchi wote.

“Alichotendewa hakustahili kutendewa sisi tunalaani vikali sana wale wote waliochukua sheria mkononi kinyume cha sheriaa hapakuwa na sababu yoyote inayohalalisha kufanya walichofanya alikuwa anafanya kazi zake kwa mujibu sheria,”amesema. 

Marehemu akiwa muajiriwa wa TRA yeye na wenzake walikuwa wanafanya kwenye kazi zao kwenye idara ya forodha