Na Mwandishi Maalum, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itahakikisha inasimamia kikamilifu shughuli za michezo ili kuliwezesha Taifa kushiriki katika michuano mbalimbali ya Kimataifa.
Dk. Mwinyi ametoa ahadi hiyo mara baada ya kukamilika kwa mchezo wa fainali wa michuano ya Soka ya ‘Yamle yamle Cup’ iliyofanyika katika Uwanja wa Amani Jijini hapa, ambapo klabu ya Mboriborini FC iliwachapa Mbirimbini goli 2-1 na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na mamia ya wapenda soka kutoka Mikoa mitatu ya Unguja, Mboriborini ilikuwa ya kwanza kupata goli dakika ya 37 lililofungwa na Ibrahim Abdalla ambalo lilidimu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili Mbirimbini ilifanikiwa kupata goli la kusawazisha lakini dakika ya 89 Ibrahim Abdalla aliwainua kwa mara nyingine mashabiki wa Mboriborini FC baada ya kuwafungia goli la pili na la ushindi.
Bingwa huyo aliondoka na kitita cha Sh. milioni 7, kombe pamoja na Jezi, huku mshindi wa pili timu ya Mbirimbini FC wakiondoka na Sh. milioni 4, Jezi na kombe pia huku Mfungaji Bora, Ali Othman Mmanga kutoka timu ya New Juve akiondoka uwanjani na zawadi ya Pikipiki.
Lakini licha ya fedha hizo za zawadi, Dkt. Mwinyi alichagia Sh. mlioni 10 kwa ajili ya washiriki wa michuano hiyo baada ya kuridhishwa na viwango walivyovionesha katika mchezo huo huku akiwapongeza waandaaji wa michuano hiyo Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na kubainisha hatua hiyo itakuza vipaji.
Pia amewataka wadau kukaa pamoja na kuondoa vikwazo vyote vinavyokwaza maendeleo ya michezo nchini ikiwemo soka, hatua itakayoleta ufanisi katika michezo.
“Nawashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi uwanjani kushangilia mchezo huu na kwani hii inatoa taswira ya mapenzi makubwa waliyonayo katika soka. Nawapongeza
Mashirika na taasisi mbali zilijitokeza kudhamini michuano hiyo, ikiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF), Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Yassin Professional, ZAT, Shirika la Bima, Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) pamoja na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),” amesema Dkt. Mwinyi.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania