Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Maonyesho ya Kilimo – Nane Nane 2023 yanatarajiwa kufunguliwa leo tarehe 01.08.2023 katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya ambapo mgeni rasmi wa sherehe hizo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Sunday Deogratias, wamewasili Jijini Mbeya kwaaajili ya kushiriki zoezi la ufunguzi wa maonyesho hayo.
Wamefanya ukaguzi wa mwisho wa Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa- ambalo limekamilika tayari kuwapokea viongozi, wadau wa kilimo na wananchi wote kiujumla kulitembelea banda hili ambalo limejipambanua kwenye;Maonesho ya bidhaa za Kilimo kwa mifano ya mazao mbalimbali yanayozalishwa Ludewa (Shamba Darasa na Bidhaa zake).Bustani ya kisasa ya mbogamboga.
Bwawa la Samaki la Kisasa lenye aina mbalimbali ya Samaki wanaofugwa kupitia programu za Ufugaji wa Samaki Wilayani Ludewa- ambapo yupo mfugaji wa Mfano kutokea Wilayani Ludewa.Kuku ambao wanafugwa Wilayani Ludewa na mfugaji wa Mfano kutokea Wilayani Ludewa.
Bidhaa mbalimbali za Kilimo; Ufugaji, Ujasiriamali kutoka Ludewa. Muongozo wa Fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana Ludewa.
Maonyesho hayo kwa mwaka 2023 yameambatana na kauli mbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mfumo endelevu wa chakula”.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini