Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online, Zanzibar
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameungana na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi katika dua na kumbukizi ya miaka 53 ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Dua hiyo imefanyika Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar,Aprili 07,2025,ambayo imeongozwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge Mussa Zungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid,.

Huku wengine ni Marais Wastaafu wa Zanzibar Ali Mohamed Shein na Amani Abeid Karume, Mjane wa Hayati Abeid Karume Mama Fatma Karume pamoja na familia ya Hayati Karume.
Pia Wengine waliohudhuria ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Stephen Wasira, viongozi,wanachama na wazee wa CCM,viongozi wa Mahakama, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi wa dini mbalimbali.



More Stories
Diwani awapa bima za afya watoto wa mahitaji maalum
Rais Mwinyi:Tuzindue mpango wa ujuzi kwa vijana katika uchumi wa buluu
Wasira:Ilala kuna watu wameanza kampeni