Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe ameutaka uongozi wa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kuendelea kuwajengea uwezo wataalamu walio katika ngazi ya msingi kwa lengo la kuwaongezea ujuzi katika kutoa huduma bora.
Aidha Dkt .Magembe ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa jitihada kubwa zinazofanywa katika uboreshaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo.
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema hayo leo mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Mbeya ambapo amesema uongozi wa hospital na watumishi kwa kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wa Nyanda za Juu Kusini.
“Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayofanya, tunaona jinsi wananchi wanavyowapongeza,pia tunaona utayari na uharaka wenu tunapowaletea changamoto za wananchi huwa mnakuwa wepesi kuzitatua ,” Dkt. Grace Magembe.
Amesema kuwa pamoja na kazi kubwa wanayofanya bado wana jukumu la kuzijengea uwezo hospitali za wilaya na vituo vyote vilivyoko katika ngazi ya msingi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameishukuru serikali kupitia wizara ya afya kwa uboreshaji wa miundombinu , vifaa tiba ikiwemo mashine ya MRI na kuhaidi kuyafanyia kazi yale yote aliyoelekeza Dkt. Magembe.
“Tutaendelea kushirikiana na wenzetu, sisi kama hospitali ya Kanda Mbeya, ni wajibu wetu kuwajengea uwezo hospitali za Wilaya na ngazi ya msingi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma zilizo bora,” Dkt. Godlove Mbwanji.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imeendelea kuboresha huduma zake ikiwemo huduma za mionzi na huduma za vipimo vya MRI pamoja na huduma za afya ya mama na mtoto.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu