Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amepiga marufuku ubadilishaji matumizi katika halmashauri nchini usio na tija.
Dkt Mabula alipiga marufuku hiyo alipotembelea eneo lenye mgogoro lililokuwa shamba la NARCO Gezaulole kata ya Somangila Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari 2023.
Amesema, kumekuwa na tabia ya kubadilisha matumizi usio na tija alioueleza kuwa unaharibu mija na mipango inayowekwa na halmashauri kupitia mipango kabambe pamoja na yeye kulipiga marufuku mara kwa mara.
Kwa mujibu wa Dkt Mabula, ubadilishaji matumizi kwenye maeneo unafanywa na halmashauri husika na utaratibu wowote wa kubadilisha matumizi usiozingatia taratibu unaenda kinyume na mipango miji sambamba na kuharibu miji.
Akitolea mfano wa Manispaa Kigamboni. Dkt Mabula alisema manispaa hiyo inao mpango kabambe ambapo mipango yote katika halmashauri hiyo inatakiwa kuzingatiwa ama kutekelezwa na kushangazwa kabla ya kutekelezwa mpango huo matumizi yanaanza kubadilishwa.
‘’Hapa mnayo master plan inayotakiwa kutekelezwa na haijaanza katika utekelezaji lakini mnaaza kubadilisha matumizi maana yake katika uandaaji hamkuwa na uhakika manapanga nini, hii haiwezekani’’ alisema Dkt Mabula
Ametaka matumizi ya ardhi katika manispaa ya kigamboni kubaki kama yalivyopangwa na kama kuna uhitaji wowote wa lazima basi ni lazima ufahamike kama ni wa mamlaka au ni wa mtu binafsi.
Awali Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile alimueleza Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula kuwa, katika jimbo lake kumekuwa na tabia ya ubadilishaji matumizi usio na tija alioueleza kuwa, kwa kiasi kikubwa unachangiwa na baadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi.
‘’Hapa kigamboni kumekuwa na ubadilishaji matumizi na watu wanavamia mpaka maeneo ya public na hili linachangiwa na baadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi hili nakuomba mhe Waziri ulipige marufuku’’ alisema Dkt Ndugulile.
Dkt Mabula alitembelea eneo ya lililokuwa shamba la NAFCO Gezaulole kata ya Somangila manispaa ya Kigamboni baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wa eneo hilo. eneo hilo limeingia mgogoro na baadhi ya wananchi kwa madai kumiliki kihalali eneo hilo.
More Stories
Wanafunzi 3000 wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Rais Samia, Mwinyi ‘mitano tena’ Nchimbi aula
Dkt.Kikwete:Ushindi wa CCM ni lazima