Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MWENYEKITI Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dkt.Jakaya Kikwete amesema kwa mipango mizuri iliyopo katika Chama hicho ushindi wa viongozi kwa nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu ujao ikiwemo ya ngazi ya Urais kupitia chama hicho ,ni lazima.
Huu ni mwaka wa Uchaguzi wa Rais,Wabunge na madiwani ambao unatarajiwa kufanyika mwishoni mwaka huu.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho Dkt.Kikwete amesema pamoja na matarajio makubwa ya ushindi wa chama hicho lakini umakini unahitajika na siyo kubweteka.
Amesema,mbali na wagombea wa CCM ambao wajumbe wamewapendekeza kugombea nafasi ya kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Dkt.Hussein Ally Mwinyi kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,lakini pia kutakuwepo na wagombea Kutoka vyama vingine na hakuna namna watakavyoweza kushinda
“Lakini hata hivyo tujiandae kwamba tunaenda vitani ,siku zote unapoenda vitani lazima ujue vita ni kubwa hata kama una Imani utashinda.”amesema Dkt Kikwete
Amewaasa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwenda kuwaeleza wananchi yaliyofanywa na CCM Ili waweze kuchagua viongozi wanaotokana na chama hicho.
More Stories
Wanafunzi 3000 wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Mkutano Mkuu maalumu CCM wapitisha Rais Samia ‘mitano tena’
Hoja ya Lusinde yawaibua wagombea Urais ,wajumbe washangilia