January 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Kikwete:Elimu ya masuala ya kisheria bado inahitajika kwa wananchi

Na Joyce Kasiki ,Timesmajira online,Dodoma

RAIS Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete amesema bado kuna umuhimu mkubwa wa elimu na msaada wa masuala ya kisheria kutolewa kwa wananchi Ili wapate uelewa wa kutosha wa masuala ya kisheria.

Akizungumza jijini Dodoma katika uzinduzi wa wiki ya Mahakama,Dkt.Kikwete amesema wiki hiyo itumike kikamilifu kutoa Elimu hiyo ya masuala ya kisheria kwa wananchi.

Amesema ,wananchi watakaohudhuria katika mabanda yaliyopo katika viwanja vya Nyerere ,watakuwa na mengi ya lujifunza kuhusu huduma za haki.

“Wiki ya Mahakama ni jukwaa muhimu la kujitathmini kwa utendaji wa Mahakama lakini pia kutoa Elimu kwa umma kuhusu masuala ya Sheria

Amesema Mahakama ni muhimili ambao unaweza kushiriki kikamilifu katika kutoa mchango kwenye dira ya maendeleo ya 2050 huku akisema ,jamii iliyokosa Utawala wa kisheria na haki haiwezi kufikia Maendeleo ya kiuchumi na kijamii .

Aidha amesema , maboresho ya utoaji haki katika Mahakama ni mafanikio mkubwa sana nchini huku akisema hivi sasa karibu mikoa yote ina Mahakama Kuu na wilaya zote 139 Zina Mahakama za wilaya .

Vile vile ametoa pongezi kwa ubunifu wa Mahakama katika utoaji huduma ikiwemo matumizi ya mifumo ya kielektroniki na Mahakama tembezi katika utoaji haki kwa wananchi.

Awali Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof Ibrahim Hamis Jumaa amesema wiki hiyo hutumika kutoa elimu ya Sheria kwa jamii na kuiwezesha kufahamu katiba ,kanuni na tararibu na kufahamu shughuli za Mahakama na haki madai .

Amesema kilele Cha Wiki hii ni Februari 3,mwaka huu ambapo Rais Dkt.Samia atahitimisha wiki hiyo .

Maadhimisho ya wiki ya Mahakama yanaongozwa kauli mbiu isemayo ‘Tanzania ya mwaka 2050 nafasi ya taasisi zonazosimamia haki katika kufikia malengo ya dira ya Taifa ya 2025’

Ameitaka Mahakama na taasisi zake zote zifanye maboresho katika Utekelezaji wa dira ya 2050 lakini pia ametaka wiki ya Sheria itumike kukumbushana kuhusu mambo mapya ya Utekelezaji wa dira ikiwemo Utawala Bora, Amani na Utulivu kwa kuangalia Sheria ,sera na miongozo kama inaakisi dhana ya utawala Bora.