Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,OnlineDar
WAZIRI wa Nishati, Dk.Medard Kalemani, leo (Julai 4) amefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua shehena ya Transforma sita zilizo wasili kwa ajili ya kupelekwa katika Mradi wa umeme wa Megawati 2115 wa Julius Nyerere.
Akikagua Transforma hizo, Dkt kalemani amesema lengo la ziara yake ni kuhakikisha taratibu zote za kutoa mzigo wa Transforma hizo bandarini zinakamilika kwa wakati ili kuwezesha Mkandarasi aliyeko katika Mradi wa Julius Nyerere kukamilisha kazi ya ufungaji transforma hizo kwa muda ulio panga.
“Nataka mchakato wa kuondoa na kusafirisha transfoma sita zilizowasili kwa ajili mradi wa Julius Nyerere, ukamilike , na itakapo fika Julai 12,2021 Transfoma zote ziwe zimetolewa”
Dkt. Kalemani ameitumia fursa hio kuwaagiza wataalamu kutoka Wizara ya Nishati kufanya maandalizi ya kutoa mizigo hii muhimu mapema iwezekanavyo ili kuondoa usumbufu wa mitambo kukaa muda mrefu bandarini na kuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi.
Hadi sasa transfoma hizo sita kati ya transfoma 29 zinazohitajika katika mradi wa Julius Nyerere zimesha wasili bandari ya Dar salam na kuanza kusafirishwa kuelekea eneo la mradi.
Shehena nyingine inatarajiwa kuwasili Julai 15, 2021 , Agosti 15, 2021 na Septemba 15, 2021 alisema Dkt. Medard Kalemani.
Serikali kupitia Wizara ya Nishati tayari imeshatuma wataalam nje ya nchi kukagua mitambo Mingine ya kuzalisha umeme (turbines) ili kujiridhisha kama zinatengenezwa kwa viwango kulingana na mahitaji .
Dkt alimaliza kwa kusema mwezi Mei, mwaka 2022 utakuwa ni mwezi wa kufanya majaribio, matayarisho na matengenezo ya kufunga mitambo ya kuzalisha umeme (turbines) kabla ya uzinduzi rasmi wa Mradi huo unao tarajiwa kufanyika mwezi Juni, 2022.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa