Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dkt. Anna Henga (Wakili) amelazimika kusafiri umbali wa Km 1,500 kumfuata aliyekuwa Ngariba wa ukeketaji mkoani Tarime, Bhoke Ryoba 66 aliyetekeleza ukeketaji kwa mabinti zaidi ya 2,000 kwa miaka kumi alivyofanya kazi hiyo.
Ngariba huyo anaishi Katika kijiji cha Masanga ,kata ya Nyamwale, wilayani Tarime Mkoani Mara aliachana na shughuli hiyo tangu mwaka 2015 huku akikiri alifanya hivyo akiamini yupo sahihi.
Dkt. Henga alichukia uamuzi huo baada ya kutonywa na Asasi ya Kupinga Ukeketaji (ATFGM) iliyoko mkoani huko alitaka kujua sababu ya Bhoke kutekeleza hilo ilihali ni kinyume cha seheria.
Ameelezea kuhusu kutekeleza biashara hiyo, Bhoke alisema jamii ya Wakurya wanaheshimu na kuenzi ukeketaji na endapo angeachana na shughuli hiyo mapema angeweza kupoteza maisha.
Amesema alikuwa anafanya hivyo ili kuwasaidia mabinti waweze kuolewa bila shida na kujipatia fedha ambazo zimemsaidia kujenga nyumba mbili na kusomesha watoto.
“Gharama ya kulipia zoezi la ukeketaji ni Sh 10,000 na hiyo ni kwa miaka ya 2008 na kwa wakati huu gharama inafika mpaka Sh 20,000 kwa msimu wa ukeketaji huwa tunakeketa zaidi ya mabinti 200 na wazazi wao lazima walipie fedha na zinagawanywa kwa wazaee wa Mila na Mangariba.
“Nilikuwa sijui kama kukeketa ni kosa kisheria jamii ya huku wanaamini binti asipokeketwa anakuwa hajatimia ndio maana hii mila badoa inaendelea huku kwa kifupi huu ni mradi wa mangariba kujipatia fedha” alisema Bhoke akiwa nyumbani kwake alipohojiwa na Dk Anna kuhusiana na harakati hizo.
Hata hivyo Dkt. Henga alionya kitendo cha baadhi ya Mangariba kubadili ukeketaji kuwa mradi huku akiitaka jamii kutokuutumia kama kivuli cha kujipatia fedha akisisitiza kitendo hicho ni ukatili wa kijinsia na kinakatisha ndoto za mabinti wengi.
“Jambo hilo limekuwa likisababisha madhara mengi ikiwemo kukatisha masomo, ndoa za utotoni,vifo kwa watoto hasa wakati wa kujifungua pamoja na kuchochea magonjwa mbalimbali” amesema Dkt. Henga
Mkoa wa Mara hasa jamii ya Wakurya umekuwa ukiendelea kuenzi mila ya ukeketaji kwa miaka ambayo inagawanyika kwa mbili na wamekuwa wakifanya maandalizi makubwa katika kutekeleza zoezi hilo ambayo huanza Agosti na ukeketaji hufanyika Desemba.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja