November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Gwajima ataka  watumishi kuwajibika kikamilifu

Na Penina Malundo,Timesmajira Online

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima ,amewataka Watumishi wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi  jamiikuongeza uwajibikaji katika majukumu yao huku akiwataka wadau na wanaharakati wa kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia  kupeleka taarifa zao kwa Maofisa Ustawi pamoja na Maofisa Maendeleo ya Jamii  wa Mikoa ili ziweze kufanyiwa kazi.

Akizungumza hayo juzi Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Waziri Dkt.Gwajima alipokutana  na wadau kutoka shirika la WILDAF na  Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia(Mkuki coalition) kuzungumzia masuala mbalimbali ya ukatili wa kijinsia katika makundi mbalimbali ikiwemo watoto.

Dkt.Gwajima amesema kuanzia April 15 mwaka huu kwa kushirikiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) ,Bashungwa serikali inatarajia kutenga wiki maalumu kwaajili ya ya kupokea taarifa za mikoa yote nchini  juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia.

Amesema kwa kupitia wiki hizo maalum itasaidia kwa kiasi kikubwa Serikali kupata taarifa sahihi za masuala hayo na kuhakikisha inashughulikia ili kuweza matatizo ya ukatili wa kijinsia nchini.

Aidha amesema zoezi hilo pia  litakuwa ni kipimo cha kuangalia changamoto zilizopo na  nani anatekeleza majukumu yake na ambaye hayatekelezi kwa 

Maofisa Ustawi pamoja na Maofisa Maendeleo ya Jamii.

“Kuanzia  tarehe 15 Aprili nitaongea na Waziri mwenzangu  Bashungwa  tutakuwa na wiki ya kupokea taarifa za Mikoa ambapo tunaamini hadi taarifa zitufikie mtakuwa mmeshaongea na Maofisa Maendeleo ya Mkoa na Ustawi mtuletee hiyo taarifa  hatuhitaji hata kukutana tutatumia Zoom “amesema 

Kwa Upande wake  Mwenyekiti wa Bodi ya WilDAF,Dkt.Monica Mhoja  amesema WilDAF inatambua dhamira ya serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa wanawake na watoto dhidi ya vitendo vya ukatili hivyo WilDAF itashirikiana bega kwa bega.

Amepongeza Waziri Dk.Dorothy kwa kutenga muda wake na kutembelea WilDAF na kahiadi kuteleza maagizo na maelekezo yote yanayotolewa na serikali.

Aidha amesema wanaomba sera ya Jinsia ikamilishwe na kuzinduliwa ili kuweza kusaidi kumaliza tatizo la ndoa ya utotoni kwani bado zipo kwa baadhi ya makabila