Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Nabii Mkuu Mheshimiwa Balozi Dr. GeorDavie K. Moses, Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Jijini Arusha, ameteuliwa rasmi na Shirika la Mabalozi wa Amani la Umoja wa Mataifa UN-PAF kuwa Mwakilishi na Balozi wa Afrika Mashariki.
Mara baada ya uteuzi huu kufanyika jijini New York nchini Marekani tarehe 9.9.2025, Mwenyekiti wa Dunia wa UN-PAF, Mhe. Balozi Kingsley Ossai, ametuma barua za Utambulisho rasmi kwa Serikali ya Tanzania pamoja na United Nations chapter ya Tanzania na Ubalozi wa Marekani nchini, kwa dhumuni la kumtambulisha Mhe. Dr. GeorDavie katika wadhifa wake mpya.
Dkt. GeorDavie ambaye pia ni mlezi wa JMAT Taifa, amekuwa akifanya kazi za Ubalozi wa Amani na kugusa maisha ya watu mbalimbali hasa katika suala zima la kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kielimu na hivyo kumfanya aendelee kuwa nuru na alama ya amani, upendo na kung’ara kimataifa kutokea nchini Tanzania.
Tunaamini kama Balozi wa Amani Duniani, ataziwakilisha vema nchi za Afrika Mashariki kupitia Shirika hilo la Mabalozi wa Amani wa Umoja wa Mataifa / UN-PAF.

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi