Na Esther Macha,Timesmajira, Online, Mbeya
SERIKALI mkoani Mbeya imeisisitiza Taasisi isiyokuwa ya kiserikaliChild support inayojishughulisha na masuala ya watoto wenye ulemavukuhakikisha inaendelea na zoezi la kuwatambua na kuwabaini ,kuwalinda watoto wote hasa wenye ulemavu ili kujenga Taifa lenyeusawa na usalama na jumuishi kwa wote na vizazi vijavyo .
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Dkt. Rashid ChuaChua wakati wa hafla ya kukamilisha mradi wa kuboresha mazingirajumuishi na salama kwa watoto wote Tanzania unaodhaliliwa na ubaloziwa Ujerumani nchini Tanzania kupitia shirika la Child SupportTanzania.
Dkt. Chuachua amesema kuwa kuna kundi kubwa la watoto hivyo Childsupport iendelee na zoezi la kuwatambua watoto wote wenye mahitajimaalum ili waweze kupata elimu ,watoto ni wengi lakini tuombemuendelee kutusaidia kwa kiasi kubwa ili kuokoa kundi hili la watotowenye ulemavu .
Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa hata kama Child supporthawataweza kuwafikia watoto wote lakini wajitahidi kufanya stadi kubwaya kuipa serikali kuwa watoto wenye mahitaji maalum ni kiasi Fulani .
“Inawezekana msiweze kufikia watoto wote na kuwafikia sababu ya uwezowenu wa kuwahudumia watoto hawa kwenye taasisi yenu na namna yakuwafikia lakini mfanye stadi kubwa kwani inawezekana mkoa mzima yakuipa picha serikali ya mkoa na kuwasilisha kwa mkuu wa mkoa ,kwambabaada ya kufanya utafiti watoto wenye mahitaji maalum ni hawa”amesema.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo nikutokuwa takwimu za watoto wenye mahitaji maalum kuna changamotokubwa za takwimu za watoto wenye ulemavu takwimu zetu zinazeeka nakupitwa na wakati unaweza ukute hata ofisa maendeleo ya jamii wamkoa nikimwita hapa akaja na takwimu za miaka mitano iliyopita mpakamiaka kumi .
Hata hivyo Dkt. Chuachua amewataka Child Support Tanzania kuja nampango mkakati wa kufanya stadi ya kuwa na taarifa sahihi za sasa zawatoto wangapi wenye ulemavu na mtasaidia na wengine wanaohitajikufanya kazi kama yenu na kuwa sehemu ya mradi wa taasisi .
Aidha amesema kuwa kuna changamoto ya lishe child support mfanye stadina baadhi ya changamoto za mtindio wa ubongo na udumavu zinatokana nalishe na lishe kuanzia mtoto akiwa tumboni suala la lishe mlifanyiekazi ,mkikaa na madaktari wanaweza kueleza kuwa baadhi ya watotomnawaowahudumia wanatokana uduni wa lishe toka wakiwa tumboni .
“Pia niwahahakishie wadau wa elimu wote na wananchi wa mkoa wa mbeya mbako mradi huu umegusa kuwa mkoa wa mbeya na serikali kwa ujumlatumedhamilia kwa dhati kabisa kuhakikisha kuwa changamotozinazowakumba watoto wenye ulemavu wote zinapatiwa suluhu na hudumastahiki ikiwa na kuhamasisiaha utambuzi na usajili wa watoto haokatika mfumo rasmi wa elimu nav takwimu ili wapate haki zao nahuduma mbali mbali za kijamii kwa kuwalinda na kuwashirikishaipasavyo katika maendeleo ya Taifa,amesema .Noela Msuya ni Mkurugenzi wa Shirika la Child Support Tanzania “amesema.
kuwa katika upatikanaji wa elimu jumuishi kulikuwa uhaba wa vifaakulingana na mahitaji ya watoto ,mifumo ya elimu na upimaji, uchunguzi na ubainishaji, mitihani naupangaji wa madaraja.
Aidha Msuya alisema kuwa pia wamepata mafanikio katika elimu jumuishikwa kutoa elimu na usalama jumuishi kwa walimu 26 kwa shule sitaambazo ni Homboro,Buigiri Dodoma, malangali Rukwa, mkuyuni , naChild Support Tanzania School na Katumba 2 Mbeya iliyopo wilayaniRungwe.
Kwa upande wake Ofisa elimu maalum Mbeya Jiji ,Wende Mbilinyi amesemakuwa taasisi hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa mkoa wa Mbeya hata kwaserikali imekuwa ikisaidia kwa kiwango kikubwa mambo yote ya childsupport Tanzania yataendelea kufanyiwa kazi na serikali .
More Stories
Tanzania,Uturuki kushirikiana kuinua sekta ya utalii nchini
Wanaoficha watoto wenye ulemavu kusakwa
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu