April 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Biteko:Wananchi someni taarifa za nishati kutoka EWURA

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online,Dodoma

Wananchi wametakiwa kusoma kwa kina taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati (umeme,petroli na gesi asilia) nchini,zinazoandaliwa na kutolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).Wananchi Someni Taarifa za Nishati”

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko,wakati wa hafla ya kuzindua taarifa hizo, iliyofanyika jijjni Dodoma, Aprili 9,2025.

Dkt.Biteko,amesema, wananchi wazisome taarifa hizo ili kubaini changamoto na fursa zinazopatikana katika sekta ya nishati pamoja na hatua zilizochukuliwa na Serikali kutafuta suluhu ya changamoto husika.

Sanjari na hayo ameipongeza EWURA,kwa kuandaa taarifa hizo,ambazo amesisitiza kuwa ni kioo cha kujipima na kutathmini ufanisi wa utendaji wa sekta hiyo katika kuwahudumia wananchi na watoa huduma.