May 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Biteko:Tanzania yadhamiria kuendeleza mageuzi ya kidigitali katika elimu

Na Penina Malundo, Timesmajira

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewahimiza wadau wa elimu barani Afrika kuendeleza mkakati na ushirikiano utakaowezesha mageuzi ya kidigitali katika sekta ya elimu.

Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Mei 8, 2025 jijini Dar es salaam wakati alipomwakilisha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Kongamano la 18 la eLearning Afrika.

Amesema Tanzania inaendeleza dhamira yake ya mageuzi ya kidigitali katika elimu na wanaendelea kushirikiana na Serikali, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na wanazuoni ili kufanya e- learning kuwezeshwa kwa ghrama nafuu kwa wote.

Amesema kuwa Tanzania imedhamiria kuongoza katika mageuzi ya kidigitali barani Afrika ambapo Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 inatambua kuwa mageuzi ya kidijitali ni kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi, maendeleo ya kijamii na ushindani wa kimataifa. Ili kufanikisha hili, Tanzania imeandaa mifumo kadhaa ikwemo Sera ya Taifa ya TEHAMA na Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali Tanzania 2024-2034.

Dkt. Biteko amesema kuwa Mkakati wa Taifa wa Elimu ya Kidijitali na Programu ya Tanzania ya Kidijitali zinalenga kuimarisha miundombinu na huduma za kidijitali, kuhakikisha teknolojia muhimu, vifaa, muunganiko na rasilimali za e-learning vinafika maeneo mbalimbali nchini, aidha nchi zingine pia zitumie rasilimali zao katika kusaidia mageuzi ya kidijitali katika nchi zao.

Amewahimiza wadau wa kongamano hilo kuwa ili mageuzi ya kidijitali ya Afrika yaweze kufanikiwa, lazima kuwezeshwa kwa nguvu kazi yenye ujuzi kuanzia umri mdogo. Tanzania imefanya marekebisho ya Sera ya Taifa ya Elimu na Mafunzo mwaka 2023 na kuwa ni mfano muhimu, ikisisitiza uendelezaji wa ujuzi kuanza elimu ya msingi.

“Sera hii pia inakuza matumizi ya teknolojia za kidijitali ili kukabiliana na upungufu wa walimu, kupanua upatikanaji wa elimu, na kuboresha ubora wa kujifunza