Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewasili mkoani Shinyanga akitokea jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi Desemba 29, 2023.
Alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kahama, Dkt. Biteko alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM)mkoani Shinyanga akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi, Mbunge wa Ushetu, Emanuel Cherehani na Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua