KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Bashitu Ally amesema wanapoelekea mwishoni mwa kampeni wanafanya kampeni kwa mtindo wa bandika bandua.
Pia amesema kama chama wamekubaliana katika kuzingatia yale ambayo waliyoelekezwa na mgombea urais wa CCM,Dkt.John Magufuli ya kuhakikisha wanafata misingi ya uhuru wa Taifa kutolegeza wala kulegezwa na mtu yeyote.
Amesema kwa sasa CCM wamezindua awamu ya tano ya mampeni ambapo mgombea urais Dkt.Magufuli atazunguka katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam.
Ameyazungumza leo jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Benjamini Mkapa katika mkutano wa mampeni wa chama hicho cha kuomba ridhaa kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
“Tangu Oktoba 2, mwaka huu Dkt.Magufuli ameingia Dar es Salaam amefanya kazi za kitaifa na leo anaanza tena kufanya kampeni kwa awamu ya tano hapa.
“Sekretarieti ilieleza ikupangie mikutano minne hapa…leo ni mkutano wa kwanza ambapo tumepanga kuwafikia wapiga kura wa majimbo matatu Kigamboni,Temeke na Mbagala,” amesema.
Aidha amesema mkutano wa pili utakuwa Kinyerezi kwa majimbo ya Segerea,Ilala na Ukonga huku mkutano wa tatu unatarajia kuwa katika uwanja wa Barafu Mburahati utahusisha majimbo ya Ubungo na Kibamba na mkutano wanne utakuwa katika uwanja wa Tanganyika Peckars kwa majimbo ya Kawe na Kinondoni.
Amesema kufanyika kwa mikutano hiyo ni kutokana na ukubwa wa jiji hilo na kuweza kuwafikia wapiga kura wengi.
“Sasa tunaenda kwa mtindo wa bandika bandua na tumekubaliana katika kuelekea mwisho wa kampeni Oktoba 27,2020 tuzingatie yale uliyotuelekeza katika vikao vya chama ikiwemo kuhakikisha misingi ya taifa isilegelegee.
“Na ndiyo maana katika kipindi cha kampeni umeweza kufanya kazi za kitaifa na kuionyesha dunia kwamba Tanzania ni kisiwa cha amani, pamoja na changamoto za kisiasa zinazojitokeza bado kqmpeni zinaendelea kwa amani na usalama na hata wageni waliofika kututembelea kwa niaba yetu Rais Museveni wa Uganda na Rais wa Malawi wameridhishwa na namna tunavyoendesha kampeni zetu,”amesema Dkt. Bashiru
Amesema sifa iliyotolewa na marais hao ndio silaha ya maendeleo ya uchaguzi.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu