January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Angeline: Turejee kwenye malezi na imani kutokomeza ukatili wa kijinsia

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Katika kuhakikisha suala la ukatili wa kijinsia linatokomezwa jamii inapaswa kurejea katika malezi na kufuata misingi ya imani za dini.

Akizungumza jimboni Ilemela Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula wakati alipo kutana na wanawake wa makundi mbalimbali kutoka jimboni humo.

Ikiwa ni kundi la tatu ambalo wamepata mafunzo ya uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022, na mapambano dhidi ya ukatili yaliofanyika wilayani Ilemela mkoani hapa na kuandaliwa na ofisi ya Mbunge huyo.

Dkt.Angeline ameeleza kuwa masuala ya kimalezi hayawezi kufanywa na serikali pekee yake lazima pia taasisi za dini zitaingia, taasisi zisizo za serikali zitaingia na makundi mbalimbali, lengo ni kuwa na mtazamo mmoja ya kutaka kumaliza changamoto hiyo ya ukatili wa kijinsia ambayo imekuwa ni kero kwa watanzania.

“Hakuna namna nyingine isipokuwa ni kurudi kwenye malezi,imani na maisha ya kwenye jamii tutaweza kupata muelekeo mzuri wa taifa lenye maadili ambalo halina ukatili na linaloishi kwa amani na usalama,”ameeleza Dkt Angeline.

Pia ameeleza kuwa suala la ukatili katika kulikemea na kulipatia ufumbuzi kama serikali ni kulitengea eneo maalum la kuweza kushughulikia nalo ambapo Rais Samia aliamua kutenganisha Wizara ya Afya na Maendeleo ya jamii ili masuala hayo yaweze kushughulikiwa kwa urahisi.

“Waziri husika akisikia tukio ata aikiwa ameliona kwenye TV,anaenda kumuona mhanga anazungumza naye anatoa elimu,na sasa hivi kama mmeona na Jeshi la Polisi pia limeanza kusaidia hilo wanaenda shule wanawaambia watoto ukiona umeshikwa huku umefanya hivi kataa kwaio serikali imeamua kuingia kwa nguvu zote kuhakikisha masuala ya ukatili ya kijinsia yanakomeshwa,ndio maana nimeliunganisha katika mafunzo kwani ni dhamira njema ya serikali kupunguza matatizo haya,”.

Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalumu Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Sarah Lisso, ameeleza kuwa kuna ukatili wa kingono ambao wanawake wanafanyiwa huku akitolea mfano kuwa kama mwanamke au binti anahitaji kazi ili aipate mpaka hatoe rushwa ya ngono.

“Unakuta pia mwanafunzi kafeli katika mitihani yake shule inautaratibu wake kuwa mwanafunzi hawezi kwenda darasa jingine mpaka afaulu kwaio ambaye amefeili mwalimu wake ana mtaka kingono ili aweze kupanda darasa hali inayomfanya Binti kufanyiwa ukatili bila kujua na kudumaza akili yake akijua ili apande darasa basi atatumia mwili wake,”ameeleza.

Pia Lisso ameeleza kuwa ukosefu wa elimu juu ya ukatili ndio chanzo cha wanawake kufanyiwa ukatili hususani walio katika maisha duni kwani hawapati elimu hiyoAmeeleza elimu ya ukatili kwa sasa inatolewa kwa watu ambao wameisha jitambua kimaisha ili wakawe mabalozi hivyo serikali iende kwenye jamii chini kabisa ili kutoa elimu hiyo kwani ukatili mwingi unafanyika kwenye jamii zilizo chini kimaisha.

“Mimi kama mama nimekuwa nikiona ukatili ukitokea kwanza kabisa ukatili wa kiuchumi unakuta baba anafamilia yake lakini akidhi mahitaji ya familia na fedha anazopata anatumia kwenye starehe,”ameeleza Lisso.