Na Martha Fatael, timesMajira online
NAIBU spika wa bunge, Dkt Tulia Akson, ametaka timu ya wapanda mlima 155 wanaopeleka bendera ya taifa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro, kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, kulinda heshma ya taifa.
Dk Tulia amesema taifa limejijengea heshma tangu kupata Uhuru Desemba 9, 1961 hivyo Kuna kila sababu kwa wapanda mlima hao kuilinda huku wakilinda tunu za Amani, Utulivu na mshikakano vilivyojengeka kwa miaka yote.
Amesema waasisi wa taifa wakiongozwa na rais wa awamu ya kwanza,marehemu Julius Nyerere, walijenga misingi imara na kumtuma kapteni wa Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ, Alex Nyirenda kupandisha bendera mlima Kilimanjaro.
Akikabidhi bandera kwa kiongozi wa mshafara huyo, Kanali wa JWTZ Martin Msumari, Tulia ametaka heshma hiyo kulindwa kama historia ilivyoandikwa.
Aidha naibu spika amesema pamoja na wimbi la ugonjwa wa Uviko 19 bado utalii haujaathirika kiwango Cha kutisha.
“Pamoja na Uviko 19 kuyapiga mataifa mbalimbali duniani, bado watalii kutoka nje ya nchi kwa mwaka 2020 walikujazaidi ya 620,867 huku kwa mwaka 2021 wakiongezeka kwa zaidi ya laki moja” amesema
Kadhalika, Dk Tulia amewataka watanzania kuongeza idadi ya watalii wa ndani, kwani kwa sasa watalii kutoka nje ya nchi ni asilimia 94 huku watanzania ukiwa ni asilimia 5 na kutaka kuhamasisha watanzania kupenda vya kwao.
Awali mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, brigedia jenerali George Waitara, ameziomba jamii zinayozunguka hifadhi za taifa kuonyesha ushirikiano kwenye ulinzi na uhifadhi wa hifadhi hizo kwani ni vyanzo muhimu vya maji na raslimali nyingine muhimu kwa watanzania wote.
Akizumngumza na wapandaji hao, mbunge wa Vunjo Dk Charles Kimei amewataka watanzania waliowakilisha upandaji huo mlima kuwa wazalendo kwa kufukisha ujumbe uliokusudiwa huku akishukuru upatikanaji wa vijana zaidi ya 300 kwa upandaji huo pekee.
Katika timu hiyo ya wapanda mlima Kilimanjaro kupitia kampuni ya utalii Zara kwa kushirikiana na Shirika la hifadhi za taifa nchini(TANAPA), ilihusisha JWTZ, Wanahabari, Bodi ya utalii TTB, Tanapa, TFS, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na wadau wengine wa maendeleo.
More Stories
Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali
Chatanda aridhishwa mwitikio watu kujitokeza kupiga kura Korogwe TC
Wanandoa wawili wamuua mtoto wao,kwa kosa la kujisaidia kwenye nguo